Sera hii inaeleza jinsi programu ya **DeniSmart** inavyoshughulikia na kulinda taarifa zako unapotumia huduma yetu.
Mwisho wa kuhuishwa: Mei 24, 2026
DeniSmart ("sisi", "programu yetu") imejitolea kwa dhati kulinda faragha ya watumiaji wake. Tunaamini kuwa taarifa zako za kifedha ni siri yako binafsi. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako.
Muhimu: Data yako inabaki kwako
Taarifa zote za madeni unayoorodhesha, kumbukumbu za malipo ya madeni hayo, viwango vya riba, na mipango ya roadmaps unayotengeneza **haziendi** kwenye database zetu za mtandaoni. Taarifa hizi zote zinahifadhiwa kwa usalama ndani ya kumbukumbu ya simu yako ya mkononi (Local Storage).
Wakati unaposajili akaunti ya mtumiaji au unapotumia huduma ya DeniSmart Pro, server zetu zinapokea tu taarifa za msingi ili kuwezesha usajili na uthibitishaji wa malipo:
Tunatumia taarifa tunazokusanya kwa ajili ya:
**Hatuuzi, hatupangishi, wala hatugawani** taarifa zako zozote za kifedha au za binafsi na makampuni ya watu wengine kwa ajili ya matangazo au madhumuni ya kibiashara. Taarifa za watumiaji zinaweza tu kutolewa iwapo sheria ya nchi inataka kufanya hivyo kwa madhumuni ya kisheria.
Tunatumia hatua madhubuti za kiufundi na kiutawala kulinda taarifa zilizopo kwenye server zetu. Hata hivyo, usalama wa taarifa zilizopo kwenye simu yako unategemea pia usalama wa kifaa chako. Tunapendekeza kuweka nenosiri (password/pattern) kwenye simu yako ili kuzuia watu wasiohusika kusoma taarifa zako za DeniSmart.
Tunaweza kubadilisha sera hii ya faragha mara kwa mara. Mabadiliko yoyote yatakapofanyika, tutasasisha ukurasa huu na kubadili tarehe ya "Mwisho wa kuhuishwa" iliyopo juu.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera hii au kama unapata changamoto yoyote katika matumizi ya data zako na mfumo wetu, tafadhali wasiliana na Uongozi kupitia WhatsApp kwa namba: